Iliandikwa ama Twajibandika by Kannon [POEM]

Written by Allan Watima aka Kannon

0

Iliandikwa
Niache nifanye vile nataka,  ukinipa wembe labda nitajikata,
Niache niishi venye nataka, kwani shida zote zenye ntapata,
Ni ju Mungu mkuu alitaka, kwa hivyo ni njia nafuata,
Nikivuta bangi, nikifuta rangi, jua ilishapangwa mi nakuza hali,
Labda nmepewa hiki kibali, ndo nijifunze matokeo ya dhambi,
Nikifa kwa ajali,  ju nlikua mlevi chakari, mama usilie tafadhali,
Yawezakuwa ni funzo kali, kwa walevi wenye gari,
Kila kitu kina sababu, msichana uliye na adabu,
Utabaki kuwa dhahabu, ata ukipata mimba kwa taabu,
Huenda mwana akawa shubaru wa kuponya walemavu,
Na ukitoa hio mimba, yawezakuwa ni kuepuka msiba,
Mimi sitishiki ukiishi kunipiku , mi ntazidi  kuishi kwa siku,
Nikiachwa mlala hoi ju nililala hai na mwizi,
Sina shida mimi  kesho ntalewa hadi nisizi ,
Na pasta ata hio sadaka ukitumia kukaba madada,
Sina shaka,  nilimtolea Mungu, mi nitapata baraka,
Mungu ashajaza kitabu tayari, sijui niko ukurasa wa ngapi,
Na hio ndio asali  maishani, na mi ni nyuki anusaye mbali.

Twajibandika
Ewe mjinga usiyejua maisha kwa undani,
Naona wawashwa na rasha rasha ya ujana,
Rika hio ndo hupekuliwa sana na shetani,
Nikalie mbali ama uache kufumba macho mchana,
Kama imeandikwa,, wale waendao jehanamu walishapangiwa?
Yaani mwisho ni motoni, ilikuwa kabla wao kuzaliwa?
Maneno yako ni kuti ya magogo kwenye uchi wa mgongo wa uti wa utu,
Kwa sababu Mungu apenda wote, apeana maisha ili tumuabudu,
Kwa hivyo sikiza maadili, panga maisha au utahesabika kwa magugu,
Kama hutaki kupanga, watembea na visa ya visanga… Shinda hapo!!!
Kama wasadiki tu kwa kiki, baraka ijayo ni ukimwi,  shida yako!!!
Waambiwa mke  atakutoroka na wamfuata ni ka mapenzi alikukopa… Shinda hapo,  hujawai sota hadi roho!!!
Na wale mnatembea na umbea badala ya injili,  mtapata kisawa ya hio kidawa ifanyayo mlegeze  ulimi,
Nayo ni moto haiishi, mwisho hakuna ushindi, kwa hivyo  shindwa hapo!