Asante – Janet Otieno [LYRICS]

0

[Verse One]
Madhaifu yangu, mapungufu yangu, kiburi changu umenipendea nini Baba.
Ubaya wangu, (ubaya wangu), shida zangu (nazo shida zangu) umaskini wangu
Umenipendea nini Baba.

Sina cha kujivunia, sifai mbele zako
Umeamua kunipenda, niseme nini Baba yangu

{Chorus}
Asante, asante Baba,
Asante, kwa kunipenda bure
Asante, asante Baba
Asante, kwa kunipenda bure

[Verse Two]
Msalabani (msalabani) ulibeba yote (ulibeba yote)
Damu ya Yesu imeniosha mimi Baba
Sasa mimi ni mwana wako (mwana wako mmoja)
Ni mridhi wa ufalme wako Baba

Sina cha kujivunia, sifai mbele zako
Umeamua kunipenda, niseme nini Baba yangu

{Chorus}
Asante asante Baba
Asante kwa kunipenda bure
Asante asante Baba
Asante kwa kunipenda bure

You May Like :   Femi One Features Mbithi, Boondocks Gang, Dj Lyta On Gengetone 'Nyoko Nyoko'

Asante(asante baba) asante baba
(asante baba) asante(ohh)
Kwa kunipenda bure
(umenipenda mie) asante
(umenisamehea mie) asante Baba
(ohh asante) asante
Kwa kunipenda bure

Kwa kunipenda bure…x2